Kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu na kueneza Injili ya Yesu Kristo Mungu Mkuu Tanzania na nje ya nchi kufuatia AGIZO KUU LA BWANA YESU (Marko 16:15)
Dira
Kuwa Kanisa linaloweza kujiendeleza kiuchumi, na kusaidia jamii kimwili na kiroho likifanya kazi kwa umoja wa Kristo
Kauli Mbiu
Tangaza Injili ya Kristo na kuleta watu kwenye Madhabahu ya Uzima na Amani. (Malaki 2:5)
Kanisa letu
Tunayo furaha kukukaribisha katika kanisa letu lenye dhumuni la kueneza injili ya Yesu Kristo. Kanisa letu lilianzishwa tarehe 17 OCTOBER 2002, na limepata usajili chini ya namba SA 10347.Mwanzilishi na Askofu Mkuu wa kanisa letu ni Kuhani Elisante Ikaka Cheya, ambaye ametuongoza kwa busara na upendo tangu mwanzo. Kanisa letu lina makao makuu yaliyoko Arusha, mtaa wa Sama, katika kata ya Moivo, Arusha. Hata hivyo, tumeenea na kuwa na matawi mkoani Mwanza, Mbeya, na Manyara, tukiendeleza utume wetu kwa njia ya kijamii, kiroho, na kimwili.
Karibu sana kwenye familia yetu ya “LIFE AND PEACE ALTAR INTERNATIONAL CHURCH”!